DSpace Repository

Sarufi ya kinyankore na ujifunzaji wa kiswahili: mfano kutoka asasi teule jijini mbarara

Show simple item record

dc.contributor.author Kubakurungi, Kyangungu Abraham
dc.date.accessioned 2026-06-12T07:33:26Z
dc.date.available 2026-06-12T07:33:26Z
dc.date.issued 2025
dc.identifier.uri http://ir.mu.ac.ke:8080/jspui/handle/123456789/10197
dc.description.abstract Wataalam waliohusika na utafiti wa lugha wanabaini kwamba lugha ya kwanza inaathiri ujifunzaji wa lugha ya pili, na hivyo kumletea mjifunzaji wa lugha ya pili changamoto mbalimbali. Huu utafiti ulichunguza namna sarufi ya lugha ya Kinyankore inavyoathiri ujifunzaji wa Kiswahili. Aidha, ulilenga kubaini changamoto zinazowakabili wanafunzi wa Kinyankore wanapojifunza Kiswahili kama lugha ya pili, na mwisho, kutoa mapendekezo ya jinsi ya kushughulikia changamoto hizo. Huu utafiti ulikuwa na malengo maalum matatu: Kwanza, kubaini athari za Kinyankore na vile zinavyojitokeza wakati wa kusoma somo la Kiswahili ikiwa ni lugha nyingine. Pili, kuchunguza kwa nini athari hizo zinajitokeza kwa wanafunzi hao wa Kinyankore wakati wanapojifunza lugha hiyo nyingine ya Kiswahili. Lengo la tatu lilikuwa kutambua mbinu mbalimbali zinazotumika kukabiliana na changamoto hizo na kusaidia wanafunzi waathiriwa wa Kinyankore katika mchakato wa kujifunza Kiswahili. Mahali ambapo utafiti huu ulifanyika ni jijini Mbarara katika asasi za elimu zilizochaguliwa, na mtafiti alilenga asasi teule za shule za sekondari na Vyuo vikuu. Takwimu za utafiti zilipatikana baada ya kuhusisha njia mbalimbali za ukusanyaji wa data, kama vile mahojiano, majadiliano, mazungumzo, hojaji, pamoja na dodoso. Njia ya usampulishaji maalum na nasibu zilitumika kuteua washiriki waliochaguliwa. Jumla ya washiriki katika utafiti huu ilikuwa mia mbili (200). Utafiti huu ulilenga kutumia idadi hii ya washiriki ili kupata maoni yanayowakilisha kundi kubwa zaidi mkoani. Utafiti huu ulichochewa na nadharia mseto, ambayo inajumuisha nadharia kadhaa hasa ile ya Uchanganuzi Makosa, Nadharia ya Uchanganuzi-Linganuzi, pamoja na ile ya Mawasiliano. Aidha, utafiti ulifanikiwa kubainisha mbinu zinazotumika kuwasaidia wanafunzi wanaokabiliwa na taathira za sarufi ya Kinyankore wakijifunza Kiswahili. Utafiti ulibainisha kwamba wanafunzi wa Kinyankore wanakabiliwa na changamoto za kisarufi katika ujifunzaji wao wa Kiswahili katika nyanja za kimsamiati, kifonolojia, kimofolojia, kisemantiki na kimuundo. Utafiti ulionyesha kwamba wanafunzi wanakabiliwa na matatizo kadhaa ya kiisimu, mkiwemo matatizo ya kisarufi, kimaandishi, kuchanganya ndimi pamoja na changamoto katika kutafsiri vipengele vya Kiswahili kulingana na lugha ya Kinyankore. Kuhusu lengo la pili, utafiti ulitambua sababu za sarufi ya kinyankore kuathiri namna Kiswahili kinavyosomwa kwa kuzingatia vigezo vyote vya sarufi ya lugha ya kwanza, matumizi ya ala za sauti za kaa kaa, kukosekana kwa baadhi ya fonimu katika kinyankore, kufundisha vibaya kwa somo la Swahili, mazingira yasiyofaa kujifunzia somo la Kiswahili, nakadhalika. Kulingana na lengo la tatu, utafiti ulionyesha mbinu zinazotumika kukabiliana na changamoto za wanafunzi wenye asili ya Kinyankore wanapokuwa katika mafunzo ya Kiswahili. Na hizo mbinu ni pamoja na; kufundisha Kiswahili tangu utotoni, wanafunzi wa kinyankore wapewe nafasi za matumizi na mazungumzo ya Kiswahili, kuhamasisha wazazi, walimu na wanafunzi kuhusu umuhimu wa Kiswahili, kuongeza vipindi na muda wa kufundisha Kiswahili kwenye ratiba za shule, kuweka mazingira rafiki ya kujifunzia Kiswahili na kadhalika. Utafiti ulihitimisha kwamba, ijapo Kinyankore kinaathiri kujifunza somo la Kiswahili kwenye ngazi zote za kisarufi kisarufi kama vile kimatamshi, kisemantiki, kimsamiati, kimuundo na kimofolojia, athari hizo haziwezi kuzuia mafunzo ya somo la Kiswahili kuendelea. Kwa maana, Kinyankore jinsi inavyotambulika kuwa Kibantu huenda ikasaidia wanafunzi kutumia uwezo wao kuelewa jinsi matumizi na uundaji wa maneno ya lugha ya Kiswahili yanavyojitokeza. Utafiti ulihitimisha kwa kupendekeza kwa tafiti zijazo kutumia nadharia nyingine kuchunguza athari zinazojitokeza katika ujifunzaji wa lugha ya pili, pamoja na kutumia muda mwingi zaidi kuzibainisha sababu na suluhisho za kila moja. en_US
dc.language.iso en en_US
dc.publisher Moi University en_US
dc.subject Sarufi ya kinyankore en_US
dc.title Sarufi ya kinyankore na ujifunzaji wa kiswahili: mfano kutoka asasi teule jijini mbarara en_US
dc.type Thesis en_US


Files in this item

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search DSpace


Advanced Search

Browse

My Account